More Website Templates @ TemplateMonster.com - October 10, 2011!

News and Events

5th to 10th October: Climate Change Adaptation
MAFUNZO JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI YATOLEWA

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa kwa kushirikiana na GIZ-Tanzania iliendesha mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (climate change) kwa wataalamu kutoka umwagiliaji, kilimo,maendeleo ya jamii kutoka Bonde la Ziwa Nyasa na Rukwa. Katika mafunzo hayo walifundishwa mambo mbalimbali kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi. Mada zilizotolewa ni pamoja na kuona kwa jinsi gani jamii inaweza kushirikishwa kuanzia ngazi ya taifa mpaka ngazi ya chini kabisa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwenye maeneo yao. Washiriki wa mafunzo haya walipata vyeti kwa kushiriki. Katika mafunzo hayo mafunzo kwa wawezeshaji yalitolewa pia.

16th to 18th September: Annual Water Conference
BODI YA MAJI BONDE LA ZIWA RUKWA YASHIRIKI MKUTANO WA WADAU WA MAMLAKA ZA MAJI-DODOMA 2015

Watumishi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa walishiriki katika mkutano wa wadau wa mamlaka za maji uliofanyika mkoani Dodoma uliondaliwa na ATAWAS kuanzia tarehe 16/09 mpaka 18/09/2015. Katika mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa, ambapo Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa ilipata nafasi ya kuwasilisha mada mbili (2) kuhusu mkakati wa mawasiliano unavyosaidia katika usimamizi shirikishi wa Rasilimali (Communication strategy as a tool for water governance) za maji pamoja na mada kuhusu utafiti wa kina cha maji cha ziwa Rukwa ( Lake Rukwa Bathymetric survey). Mbali na mada zilizowasilishwa na ofisi yetu, kulikuwepo pia na mada mbalimbali kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji kutoka kwa wadau wengine.

08th August: Nanenane exhbition
BANDA LA WIZARA MAJI (BONDE LA MTO RUFIJI, ZIWA RUKWA NA ZIWA NYASA) LAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2015

Bodi ya maji bonde la Mto Rufiji, Ziwa Rukwa na Ziwa Nyasa zilishiriki katika maonesho ya nanenane yaliofanyika katika uwanja wa Mwakangale mkoani Mbeya. Katika maonesho hayo wataalamu kutoka ofisi za maji za mabonde walitoa elimu juu ya usimamizi shirikishi wa rasilimamili za maji, mbali na utoaji wa elimu jamii ilipata kujionea vifaa mbalimbali vinavyotumika katika usimamizi wa rasilimali za maji, kauli mbiu ya nanenane ya mwaka huu ilikuwa matokeo makubwa sasa, tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo na ufugaji. Katika maonesho haya wataalaamu toka mabonde husika walionyesha ubunifu wao kuandaa chanzo cha maji kilichovutia watu wengi, ambapo waliotembelea banda letu walipata elimu jinsi ya kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki na maji, taratibu za uchepushaji wa maji na matumizi mazuri ya maji. Maafisa maji kutoka bodi ya maji bonde la ziwa Rukwa na Nyasa walifurahia maonesho hayo na kusema kuwa hii ni elimu nzuri kwa jamii juu ya usimamizi wa rasilimali za maji.

03rd Julay: WUA study trip
JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI BONDE LA ZIWA RUKWA ZAPATA MAFUNZO

Jumuiya za watumia maji kutoka bonde la Ziwa Rukwa zilifanya ziara ya siku nne (4) katika bonde la Mto Rufiji kwa lengo la kujifunza. Lengo kuu la mafunzo hayo ilikuwa ni kuzijengea uwezo jumuiya hizi katika suala zima la usimamizi wa Rasilimali za maji. Mafunzo haya yalilenga juu ya ugawaji wa maji, ukusanyaji wa mapato, utatuzi wa migogoro, uongozi na namna ya kutunza vyanzo vya maji. Jumuiya zilizopata mafunzo haya ni wanajumuiya wa bonde dogo la mto Katuma kutoka mkoani Katavi, na jumuiya za bonde dogo la mto Myovizi, Mlowo pamoja na Ruanda kutoka wilayani Mbozi.

9th June: Bodi ya Maji
BODI MPYA YA MAJI BONDE LA ZIWA RUKWA

Waziri wa Maji Profesa Jumanne Magembe ameteua bodi mpya ya Bonde la Ziwa Rukwa baada ya ile ya zamani kumaliza muda wake. Hii inakuwa ni bodi ya tatu toka kuanzishwa kwa ofisi ya maji ya Bonde la Ziwa Rukwa mwaka 2004. Katika bodi hii mpya iliyoteuliwa kuanzia April, 2015 inajumuisha wadau waliopo katika Bonde la Ziwa Rukwa ambao ni wajumbe kutoka sekta mbalimbali bila kuwasahau wadau kutoka jumuiya za watumia maji.

Majina ya wajumbe wa bodi mpya:

Lawrence W. Mbuya, Chairman

Eng. Florence Mahay, Basin Water Officer LRBWB, Secretary

Eng. Leonard Masanja - Ministry of Energy and Mines

Eng. Maua Mgallah - District Water Engineer, Momba District

Tatu Abdalah, Water User Association Katuma River

Joseph Kakunda, PCU, Ministry of Water,

Rose Mero, Lafarge - Mbeya Cement

Given Haonga, Water User Association Myowizi River

Elibariki J. Mwendo, Zonal Irrigation Unit, Ministry of Agriculture

Juliana Nzowa, Water User Association Mlowo River

Eng. Zakaria Nyanda, Mpanda UWSA

29th May: Mabadiliko ya Tabianchi
BODI YA MAJI BONDE LA ZIWA RUKWA KWA KUSHIRIKIANA NA GIZ YAFANYA JUKWAA LA KWANZA LA MABADILIKO YA TABIA NCHI KWA WADAU

Wadu mbalimbali kutoka maeneo ya bonde la Ziwa Rukwa walikutana kwa mara ya kwanza katika jiji la Mbeya kwenye jukwaa la kwanza la mabadiliko ya tabia nchi. Katika mdahalo huo wadau walioshiriki ni kutoka asasi za kiraia (NGOs), taasisi binafsi pamoja na taasisi za kiserikali zilizopo katika bonde la ziwa Rukwa. Mada zilizojaliwa katika jukwaa hilo ni pamoja na “climate change vulnerability” iliyowasilishwa na Afisa wa Maji toka Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa, “global negotiation in climate change adaptation” iliyowasilishwa na Susane Schwan, Mr Baraka Kajange kutoka coffee and climate intiative aliwasilisha mada ambayo ilihusu namna taasisi binafsi zinavyoweza kuwa na mchango katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Mada nyingine iliyowaslishwa ilihusu athari ya mabaliko ya tabia nchi katika nchi za Africa mashariki iliyowasilishwa na Mr Till. katika jukwaa hili wadau walipata fursa ya kujadili jinsi wanavyokabiliana na mabadiiliko ya tabia nchi kwenye sekta zao, ambapo ilijadiliwa katika sekta ya kilimo, mifugo, mazingira, na rasilimali za maji.

08th and 9th of May: Mkutano Wadau wa Maji
WADAU WA MAJI WAIBUA CHANGAMOTO KWENYE USIMAMIZI RASILIMALI ZA MAJI

Wadau maji kutoka mkoani mbeya walikutana kwenye kikao cha siku mbili wilaya Rungwe kujali changamoto zilizopo katika usimamizi wa rasilimali za maji. Wadau walioshiriki katika kikao hicho ni mameja wa mamlaka ndogo za maji, wataalamu toka NEMC, Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa na Nyasa, wahandisi wa maji wilaya pamoja na wataalamu wa afya toka wilayani Rungwe. Mada zilizojadiliwa ni hali ya ubora wa maji katika mkoa wa mbeya, ushiki wa wadau mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za maji pamoja na elimu juu ya sheria ya maji. Washiriki walipendekeza kuwa ni vema suala la kuharibiwa kwa vyanzo vya maji katika sehemu nyingi hapa mkoani mbeya likasimamiwa kikamilifu. Wajumbe kwa pamoja walikubaliana kwamba ni vema kukawepo na majukwaa ya mara kwa mara katika suala zima la usimamizi wa rasilimali za maji.

16th to 22. March 15: Maji Wiki
MAADHIMISHO YA MAJI WIKI

Bodi ya maji bonde la Ziwa Rukwa kwa kushirikiana na GIZ, walihitimisha wiki ya maji 2015 kwa kishindo kupitia mashindano ya mpira wa miguu, ambapo jumla ya timu nane (8) zilizopo katika bonde dogo la mto katuma zilishiriki. Mashindano haya yaliyoendeshwa kwa msaada wa GIZ yalilenga kuhamasisha jamii iliyopo katika bonde hili katika usimamizi endelevu wa Rasilimali za Maji.

11 and 12. March 15: Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira
Alipotembelea Kiwanda cha Saruji (Mbeya Cement) na Migodi tatu katika Chunya

Waziri alitembelea Jumla ya Migodi tatu (Sunshine Gold Mining, Shanta Gold Mining na Mek One Gold Mining. Katika zara yake waziri alikuwa anaangalia jinsi migodi ilivyojipanga katika utunzaji wa mazingira. Vitu alivyokuwa anaangalia ni vitu vikuu vitatu: 1) tathmini ya athari ya mazingira (EIA), Mpango wa utunzaji wa mazingira (EMP), Tailing Storage Facility (TSF - Mabwawa ya kuhifadhia mabaki kutoka mgodini. Halafu alipotembelea Kiwanda cha Saruji Mbeya Cement. Mapungufu yaliyojitokeza: Mabwabwa ya Majitaka (Waste Water Stabilization Ponds) Hayapo katika hali ya usafi unaolidhisha hivyo yatapelekea mabwawa hayo kutokufanya jazi ipasavyo. Waziri alipendekeza mabwawa ya majitaka kufanyiwa usafi haraka iwezekanayo ili kuweza kuongezea ufanisi wa utendaji kazi wa mabwawa hayo ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

26. Jan 15: Mpango wa hifadhi wa vyanzo vya maji
Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa wakipanda miti Safu ya Mlima Mbeya

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walishiriki katika mpango wa uhifadhi mazingira na vyanzo vya maji katika safu ya mlima Mbeya. Mpango huu wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji uliozinduliwa na mkuu wa mkoa tarehe 15/01/2015, lengo kuu ilikuwa ni kutafuta ufumbuzi wa uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji katika safu za mlima Mbeya. Wadau waliohusika katika kuandaa mpango huu ni wakala wa huduma za misitu (TFS), mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Mbeya, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Halmashauri ya jiji la Mbeya na Mbeya vijijini, Shamba la miti kawetere, vyombo vya ulinzi na usalama (JKT-Itende, JWTZ-Mbalizi na Jeshi la Polisi Mkoa) na Jamii inayozunguka safu ya mlima Mbeya.
Changamoto zilizopo katika safu ya mlima Mbeya zinasababishwa na shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, ambapo athari zake ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, mmonyoko wa udongo, kupungua kwa wingi na ubora wa maji na upotevu wa viumbe hai (bionuai). Mpango huu umelenga kupunguza matukio ya moto, kuzuia uvamizi wa maeneo ya hifadhi, kukazia sheria za uhifadhi wa mazingira, kutoa elimu na ushirikishwaji wa jamii kulinda na kuhifadhi safu ya mlima Mbeya , kurudisha uoto wa asili kwenye vyanzo vya maji pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya nishati.
Shughuli za utekelezaji katika mpango huu zilizofanyika toka uzinduzi wake mwezi January ni pamoja na upandaji miti iliyo rafiki na maji kwenye vyanzo vya maji vilivyopo katika safu ya mlima Mbeya ambapo zaidi ya miche 45,000 ilioteshwa,uanzishaji wa shamba darasa katika kata ya iganzo lenye mizinga 50 pamoja na kutengeneza barabara za kuzuia moto. Utunzaji wa vyanzo vya maji ni suala muhimu kwa vile linahusisha maisha ya binadamu na viumbe hai katika maeneo husika, Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa kama msimamizi mkuu wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Ziwa Rukwa ilishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango huu.

12. Dec 14: Presentation of IWRMD II plan
Severe Climate Change Impacts on Water Resources in Lake Rukwa Basin Expected

A stakeholder workshop on the review of the Interim II Integrated Water Resources Management and Development Plan (IWRMD) revealed large changes in water availability for the regions of Lake Rukwa Basin. In the workshop held in Mbeya on 11th and 12th of December, WREM International and the Lake Rukwa Basin Water Board, which is supported by GIZ, presented their water demand projections and future water availability to about 100 stakeholders from various sectors.
According to their findings, Climate Change is expected to exacerbate water stresses throughout the basin. Although a higher average precipitation levels are expected, a higher evapotranspiration due to higher temperatures will lead to a dryer climate. In addition, more heavy rains and longer droughts are expected. Because of its hydrogeological characteristics, Lake Rukwa is very sensitize to changing climate and “can act as an indicator for global warming”, as Aris Georgakakos from WREM stated.
Katuma river and Songwe river are identified as the hotspots of climate change with severe trade-off challenges between future water demands and availability. At Katuma river, water use for irrigation will not be possible for several consecutive years, if the water demand of the wetland ecosystem of Katavi National Park are taken into account. The densely populated Songwe catchment around Mbeya will suffer from water shortages during dry seasons, mainly because of population and industrial growth.
So far Environmental flow requirements are currently unsupported, indicating alarming stresses on the environment and ecosystems. A continuation of past water use and management practices will surely escalate environmental degradation and foreclose socio-economic development. Basin Water Officer Florence Mahay underlined that the “IWRMD is an opportunity for systemic change in water management and use that must not be missed”.
Stakeholders from from all districts and regions of the basin, private companies, utilities, various government authorities and ministries, as well as Water User Associations discussed on how the gaps between future water demand and availability could be met. The meeting was hosted by Mr. Kakunda, Director of Programm Coordination Unit, Dr. Hamza Sadiki, Director of Water Resources and Mr. Mbuya, Chairman of the Lake Rukwa Basin Water Board.

Lake Rukwa Basin Facts:

Coverage: Mbeya, Rukwa, Katavi and small parts of Tabora and Singida
Total Area:
88,000 km2.:
Temperature:
25C to 30C.:
Annual mean rainfall:
1095mm:
Population:
2.5 million:

 

05 Dec 14: Annual General Meeting
Basin Water Boards meet to discuss future water resources management

In a four days annual general meeting in Mtwara from December 2nd to December 5th, the nine Basin Water Boards exchanged experiences and views on the way forward in managing Tanzania's water resources.
They presented  challenges and innovative approaches, which have been put into practice in the last year. Elaborate discussions arose from the presentations on credibility of hydrological data by Prof. Kamugisha and on low-cost bathymetrie by BWO Florence Mahay from Lake Rukwa Basin, which have been the highlights for many participants. Furthermore, the presentation on the Performance Assessment Framework, developed by Ministry of Water and GIZ received a very positive feedback.
Besides the themed and research presentations, the different consultants for the Integrated Resources Management and Development Plans used the opportunity to inform about their progress. The Minister of Water, Prof. Jumanne Maghembe, PS Futakamba and the Directors for Water Resources and PCU, Dr. Hamza Sadiki and Joseph Kakunda.

 

28th Nov 14: Board election
Lake Rukwa Basin elects a new Basin Water Board

Stakeholders from local government authorities, private companies, Government institutions, water user associations, and water utilities came together on November 28th to elect a new Basin Water Board for Lake Rukwa Basin.
The Basin Water Board is the lead water management institution in the basin. Through the Board water users and stakeholders are enabled to manage their water sources themselves in a participatory and equitable way. From January 1st 2015, the new Board will issue water use permits and police water use. It will also monitor the work of the Basin Water Office, who implements the decisions of the Board and provides technical expertise to the Board members.

The new Board will consist of three representatives from Water User Associations, one representative of the private business sector, one MD from an urban utility, two Water Engineers from districts in the basin, one representative from a ministry and the Basin Water Officer. The electorate elected and recommended suitable candidates to the Minister of Water, who will officially appoint the new board members and a chairman. It will be the forth Board for Lake Rukwa Basin. GIZ supports with a development advisor as part

 

Call Center: +255 2500028Lake Rukwa Basin 2013. All Rights Reserved